1. Chagua nguo zenye rangi za kuvutia.
nzuri sizizo za kung’aa mno, mfano, purple, black, nyeusi, nyeupe, na rangi zilizopowa kama tobacco/brown na blue
2.Ni vema kujali umbo na rangi ya ngozi yako.
Unapochagua nguo, jali zaidi kimo, mfano mrefu au mfupi, pia rangi, kwani itakufanya ujisikie vema zaidi. Watu weupe hupendeza zaidi nguo zenye rangi nyeusi, nyeupe na brown au rangi ya ugoro halikadhalika watu weusi hupendeza zaidi wakivalia nguo nyeusi.
3. Suala la viatu vinavyoendana na nguo husika.
Usichanganye rangi nyingi nyingi za viatu na nguo, pendelea kuvaa nguo na viatu rafiki, mfano, raba nyeusi na jeans nyeusi, jeans nyeusi na raba nyekundu. Mfano rubber shoes nyeusi, ladies sandles nyeusi au sleepers hufaa sana zikivaliwa na nguo nyeusi pia.
3. Chagua nguo zenye prints/chapa au maandishi unayoyafahamu Au unayoyaelewa vema.
Kuna baadhi ya watu huvaa nguo, hasa T-shirts au swetter zenye prints za ujumbe usiohusiana na events husika. Mfano unavaa nguo yenye prints kama “I know I’m your pet and you feed me lovely”, “I’m a dog brother”.au “I love my pooh”ingefaa kuelewa ujumbe ili kuepuka kuchoreka. Hii itakufanya ujiamini zaidi.
4. Suala la mazingira au tukio.
Ni vema kujali mavazi na tukio au mandhari, tunafahamu si sawa kuvalia pensi au jinsi za kuchana tunapokuwa katika hafla za kielimu, au ofisini au katika shighuli za haruai au misiba. Kuvaa namna hiyo ukiwa katika interview, au katika nyumba za ibada, ni dhahiri hutajiamini vema. Kuvaa in Fashion mfano, pensi na jinsi za wazi, inafaa zaidi katima matamasha au katika matukio mengine ya kiburudani au outings.
5. Suala la pasi, usafi wa nywele na urembo wa kucha ,kope, nyusi unahusika.
Kuna baadhi ya nguo hufaa zaidi ukifanya extraordinary decorations pia usisahau bling bling. Nguo/Mavazi yanayostahili pasi ni vema yapasiwe ili kujiamini zaidi.
Nitakuletea MAKALA YA YENYE SIRI 5 KUPIGA SELFIE, PICHA SAFI UNAYOWEZA KU SHARE POPOTE. ASANTE. KARIBU.